Papa Zakaria alikuwa Papa kuanzia tarehe 3 Desemba 741 hadi kifo chake tarehe 15 Machi 752[1]. Alitokea Ugiriki[2] au Santa Severina, Calabria, Italia, labda akiwa na asili ya Balkani.
Jina la baba yake lilikuwa Polichronios.
Alimfuata Papa Gregori III akafuatwa na Papa Stefano II[3].
Anasifiwa sana na wanahistoria mbalimbali kwa jinsi alivyokabili vizuri mazingira magumu na ya hatari[4], akiongoza familia ya Mungu kwa umakinifu na busara ya hali ya juu.
Alifaulu kupatana na Walombardi walioteka sehemu kubwa ya Italia[5] au kupunguza ukali wao, aliwaelekeza Wafaranki namna ya kutawala kwa haki na kumhimiza Pipino Mfupi kujifanya rasmi mfalme wao[6], alifanya makabila ya Kijerumani yawe na makanisa zaidi, aliunga mkono umisionari wa Bonifas huko Ujerumani[7], alidumisha umoja na Kanisa la Mashariki, alipinga sera ya kaisari Konstantino V dhidi ya picha takatifu[6], alidhibiti mwelekeo wa kutunga majina kwa malaika[8] na alikataza biashara ya watumwa mjini Roma akiwakomboa waliokwisha kuletwa[5][9][10].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite book))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite book))
: CS1 maint: location missing publisher (link)Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Zakaria kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |