Maeneo ya Waorthodoksi katika Ulaya na Mashariki ya Kati
Asilimia ya Waorthodoksi duniani nchi kwa nchi:      Zaidi ya 75%      50–75%      20–50%      5–20%      1–5%      Chini ya 1%, lakini wenye haki ya kujitegemea


Waorthodoksi ni Wakristo wanaofuata mapokeo ya Mitume wa Yesu jinsi yalivyostawi kihistoria katika Ukristo wa Mashariki upande wa mashariki wa Dola la Roma iliyoitwa pia Bizanti na nje ya mipaka yake. Leo hii ni nchi za Ulaya ya Mashariki pamoja na nchi za Mashariki ya Kati ulipoenea baadaye dini ya Uislamu.

Jina

Kanisa la Orthodoksi ni jina linalotumika hasa kumaanisha Kanisa la Kikristo linalokubali mamlaka ya kiroho ya mitaguso saba ya kiekumeni tu. Leo, hasa kwa sababu ya uhamiaji, Kanisa la Orthodoksi lipo katika dunia nzima, likijumuisha watu milioni 200 hivi, lakini bado lina idadi kubwa ya waumini katika Ulaya ya Mashariki.

Jina hilo ("Orthodoksi") lina asili ya Kigiriki likitokana na maneno όρθος ("orthos", yaani "nyofu", "sahihi") na δόξα ("doksa", yaani "rai", "fundisho") yaani "wenye fundisho sahihi".

Jina hilo lilitungwa ili kutofautisha Wakristo waliofuata mafundisho rasmi ya imani yaliyotolewa na Mitaguso ya kiekumene dhidi ya mikondo mingine ya wakati ule.

Kwa namna ya pekee jina hilo lilitumika upande wa mashariki, hivi kwamba lilipotokea farakano la mwaka 1054, likabaki kama jina maalumu la makanisa yenye ushirika na Patriarki wa Konstantinopoli (leo Istanbul katika Uturuki).

Muundo

Makanisa ya kujitegemea ya Kiorthodoksi yanayotambuliwa na wote ni kama yafuatayo:

Makanisa mengine yaliyojitenga na hayo hayajakubalika.

Uhusiano na Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki wa Mashariki

Hivi karibuni hata makanisa mengine ya mashariki yamechagua kujiita hivyo, ingawa yanaendelea kutofautiana kuhusu maazimio kadhaa ya mitaguso mikuu iliyokubaliwa na Wakristo walio wengi. Leo hii wanatofautisha kwa kutumia majina

Hata hivyo pande hizo mbili zinafanana katika teolojia, liturujia na staili za fahari za ibada zao, pia katika sheria kuhusu maaskofu (wasiooa), makasisi na mashemasi (wanaoweza kuwa watu wa ndoa), tena katika umuhimu wa umonaki na maisha ya kiroho.

Ni vilevile kuhusu Wakatoliki wa Mashariki ambao wana ushirika kamili na Papa wa Kanisa la Roma bila kuacha mapokeo ya Ukristo wa Mashariki.

Marejeo

Vitabu

Marejeo mengine

Marejeo mengine tena

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Waorthodoksi

Mahusiano na Kanisa Katoliki

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waorthodoksi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.