Papa Leo IX (21 Juni 1002 – 19 Aprili 1054) alikuwa Papa kuanzia tarehe 2 au 12 Februari 1049 hadi kifo chake[1]. Alitokea Alsace, leo nchini Ufaransa[2].
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Bruno wa Eguisheim-Dagsburg[3].
Alimfuata Papa Damaso II akafuatwa na Papa Viktor II.
Akielekea Roma kwa ajili ya kutawazwa, alikutana na abati Hugo wa Cluny na kumchukua mmonaki Hildebrando ambaye akaja kuwa Papa Gregori VII[4].
Alikuwa Papa bora kutoka Ujerumani katika Karne za Kati, akijitahidi kupambana na maovu ya wakati ule[5], ingawa kutokana na utawala wake lilitokea farakano na Kanisa la Kigiriki (Farakano la mwaka 1054)[6] .
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Leo IX kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |