Papa Marselino alikuwa Papa kuanzia tarehe 30 Juni 296 hadi kifo chake tarehe 25 Oktoba 304[1]. Alitokea Roma, Italia[2].
Alimfuata Papa Kayo akafuatwa na Papa Marcellus I.
Tangu mwaka 302, Kanisa liliteseka sana chini ya Kaisari Diokletiano, aliyechochewa na kaisari Galerius. Ilisemekana kwamba Marcellinus pia aliyumba kwa muda mfupi, ila Augustino alikanusha taarifa hiyo[2].
Ikiwa Marcellino aliuawa au kufa kwa uzee, hakuna uhakika[3].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[4].
Sikukuu yake kwa Wakatoliki ni 26 Aprili (ingawa hatajwi tena katika Martyrologium Romanum[5]) ila kwa Waorthodoksi ni tarehe 7 Juni.
![]() |
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Marcellinus kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |