Mariolojia ya Kiprotestanti inajumlisha mitazamo mbalimbali ya theolojia ya madhehebu ya Kikristo ya Kiprotestanti na viongozi wake wa zamani kama vile Martin Luther na Yohane Calvin na wataalamu wa baadaye kuhusu Bikira Maria, Mama wa Yesu.
Baadhi ya waanzilishi wa Uprotestanti kama Martin Luther[1] na Huldrych Zwingli[2] walimheshimu Bikira Maria.
Kabla yao, John Wycliffe alikuwa na msimamo wa namna hiyo [3].
Kwao suala lilikuwa si heshima kwake, bali kiwango cha kufaa cha heshima hiyo[4][5].
Zaidi ya hayo, Martin Luther alishikilia dogma kuhusu Maria kwamba ni Bikira daima na anaweza kuitwa Mama wa Mungu[6] Tena alitetea mtazamo kwamba alikingiwa dhambi ya asili, au walau aliishi bila dhambi. [7]
Karl Barth (1886–1968), mwanateolojia maarufu wa Wareformed, alishika msimamo kama wa Martin Luther[8][9]
Hadi sasa Shirikisho la Kimataifa la Walutheri linakubali kumuita Maria "Mama wa Mungu"[10].
Vilevile Ushirika wa Anglikana unashika mafundisho hayo ya mapokeo yaliyotolewa na mitaguso ya kiekumeni na kumheshimu Bikira Maria kuliko namna inavyokubaliwa na baadhi ya Waprotestanti, hasa ya madhehebu yaliyoanzishwa Marekani katika karne za mwisho[11][12]
|accessdate=
(help)
|date=
(help)