Pietà ya Michelangelo katika Basilika la Mt. Petro, 14981499.

Yesu kushushwa kutoka msalabani mara baada ya kufa na kupakatwa na mama yake, Bikira Maria, ni tukio lililofikiriwa na wafuasi wake wengi na kuchorwa au kuchongwa na wasanii mbalimbali kwa ufanisi mkubwa.

Maarufu zaidi ni sanamu ambayo ilichongwa katika marumaru na Michelangelo Buonarroti na inatunzwa katika basilika la Mtume Petro huko Vatikani.

Aina hiyo ya sanaa inaitwa kwa kawaida "Pietà", neno la Kiitalia linalomaanisha huruma.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Yesu kushushwa