Mariolojia ya Kilutheri inajumlisha mitazamo ya theolojia ya madhehebu ya Kikristo ya Kilutheri kuanzia Martin Luther mwenyewe na wataalamu wa baadaye kuhusu Bikira Maria, Mama wa Yesu.
Baadhi ya waanzilishi wa Uprotestanti kama Martin Luther[1] na
Zaidi ya hayo, Martin Luther alishikilia dogma kuhusu Maria kwamba ni Bikira daima na anaweza kuitwa Mama wa Mungu[2] Tena alitetea mtazamo kwamba alikingiwa dhambi ya asili, au walau aliishi bila dhambi. [3]
Kwake suala lilikuwa si heshima kwake, bali kiwango cha kufaa cha heshima hiyo[4][5].
Hadi sasa Shirikisho la Kimataifa la Walutheri linakubali kumuita Maria "Mama wa Mungu"[6].