Picha ya ramani ikionesha eneo la Kaunti ya Nyamira, Kenya
Nyamira, Kenya

Kaunti ya Nyamira ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 605,576 katika eneo la km2 897.3, msongamano ukiwa hivyo wa watu 675 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Nyamira.

Utawala

Kaunti ya Nyamira ina maeneo bunge yafuatayo[2]:

Eneo bunge Kata
Borabu Mekenene, Kiabonyoru, Esise, Nyansiongo
Kitutu Masaba Rigoma, Gachuba, Kemera, Magombo, Manga, Gesima
Mugirango Kaskazini Itibo, Bomwagamo, Bokeira, Magwagwa, Ekerenyo
Mugirango Magharibi Nyamaiya, Bogichora, Bosamaro, Bonyamatuta, Mugirango Mjini

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019)

Tazama pia

Tanbihi

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  2. http://countytrak.infotrakresearch.com/Nyamira-county/
  3. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.