Waogiek (kwa jina lingine Waokiek au Waakiek, ingawa jina Akiek hutambulisha hasa tawi mojawapo la kabila hilo; waliitwa pia Wandorobo -tar. chini-), ni kabila la Waniloti linalopatikana kaskazini magharibi mwa Tanzania, kusini mwa Kenya (kwenye Msitu wa Mau), na magharibi mwa Kenya (kwenye msitu wa Mlima Elgon).

Mnamo mwaka wa 2000 idadi ya Waogiek ilikadiriwa kuwa 36,869, ingawa waongeaji wa lugha ya Kiakiek, mojawapo ya lugha za Kiniloti, walibaki kuwa takribani watu 500 tu [1]. Waogiek wengi wamebadilisha lugha zao hadi zile za wakazi wanaowazunguka: Waakiek kaskazini mwa Tanzania kwa sasa wanaongea lugha ya Kimaasai nao Waakiek walio Kinare,Kenya, wanaongea lugha ya Kikikuyu.

Waogiek ni baadhi ya kundi la makabila walio wawindaji-wakusanyaji nchini Kenya na Tanzania ambao kwao jina Dorobo or Ndorobo (jina lenye asili ya Kimaasai ambalo kwa sasa linachukuliwa kama tusi) limetumika.

Mizozo ya mashamba

Waogiek mara nyingi wametoa malalamiko yao dhidi ya serikali ya Kenya kwa kutoshughulikiwa matakwa yao, haswa kwa kunyang'anywa mashamba yao kwa njia haramu.[2]

Tanbihi

  1. [1]
  2. Kimaiyo, Towett J. (2004). Ogiek Land Cases and Historical Injustices — 1902 – 2004. Nakuru, Kenya: Ogiek Welfare Council. uk. 127 pages + appendices. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-29. Iliwekwa mnamo 2009-12-30.  (Maandishi timilifu kuhusu kitabu kwenye kiongu.)

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waogiek kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waogiek kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.