Songwe ni jina la mito miwili ya Tanzania: mmoja uko katika mkoa wa Mbeya, mwingine katika mkoa wa Songwe.
Songwe ya Kusini ina chanzo chake katika milima ya Umalila karibu na Santilya ikielekea kusini na kuishia Ziwa Nyasa. Baada ya kupita Itumba (Ileje) mto ni mpaka kati ya Tanzania na Malawi.
Tabia yake ya kubadilisha-badilisha mwendo wake imesababisha matatizo kati ya nchi jirani kwa sababu mashamba ya watu yamepatikana mara upande mmoja mara upande mwingine wa mpaka wa kimataifa.
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Songwe (Mbeya) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |