Kitaumande | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Kitaumande miraba
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Vitaumande ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali wa nusufamilia Surniinae katika familia Strigidae. Ndege hawa ni wadogo kuliko bundi (sm 12-28) na wana rangi ya kahawa au kijivu pamoja na miraba au madoa.
Vitaumande hula panya na wanyama na ndege wadogo wengine na hata watambaazi wadogo, popo, samaki, wadudu na nyungunyungu. Kulingana na spishi huwinda wakati wa alasiri au alfajiri au hata mchana na pengine usiku.
Jike huyataga mayai 2-7 katika tundu lililoachwa na ndege au mnyama mwingine, mara nyingi lile la kigong'ota au zuakulu. Spishi fulani huchimba vishimo katika ardhi au nyingine hutaga ndani ya matundu katika miamba, kingo za mito au majengo makuukuu au hata ndani ya vishimo vya sungura.