Bundi-panga
|
Bundi-panga Kaskazi (Surnia ulula)
|
Uainishaji wa kisayansi
|
Himaya:
|
Animalia (Wanyama)
|
Faila:
|
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Nusufaila:
|
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
Ngeli:
|
Aves (Ndege)
|
Oda:
|
Strigiformes (Ndege kama bundi)
|
Familia:
|
Strigidae (Ndege walio na mnasaba na bundi)
|
Nusufamilia:
|
Surniinae (Ndege walio na mnasaba na bundi-panga)
|
Jenasi:
|
Mascarenotus Mourer-Chauvire, Bour, Moutout & Ribes, 1994
Ninox Pennant, 1769
Sceloglaux Kaup, 1848
Surnia Duméril, 1805
Uroglaux Mayr, 1937
|
Spishi:
|
Angalia katiba
|
|
Bundi-panga ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali za nusufamilia Surniinae katika familia Strigidae.
Wengi baina ya ndege hawa wana ukubwa wa bundi, lakini wengine ni wadogo zaidi na wengine wakubwa zaidi.
Wana rangi ya kahawia au kijivu na wengi wana miraba kwa kidari kama vipanga (hii na jinsi yao ya kuwinda ni sababu za jina lao). Spishi ndogo hula wadudu hasa, lakini spishi kubwa huwinda wanyama, ndege na watambaazi pia. Huwinda wakati wa jioni, usiku na alfajiri na pengine mchana. Mara nyingi wamfukuza windo lao kama kipanga.
Jike huyataga mayai 2-6 katika shimo ndani ya mti.
- Mascarenotus grucheti, Bundi-panga wa Réunion (Réunion Owl) - imekwisha sasa (karne ya 17)
- Mascarenotus murivorus, Bundi-panga wa Rodrigues (Rodrigues Owl) - imekwisha sasa (kati ya karne ya 18)
- Mascarenotus sauzieri, Bundi-panga wa Morisi (Mauritius Owl) - imekwisha sasa (kati ya karne ya 19)
- Ninox cf. novaeseelandiae (New Caledonian Boobook, mwisho wa Quaternary) – labda inaishi bado
- Surnia capeki (Mwanzo wa Pleistocene)
- Surnia robusta (Mwisho wa Pliocene mpaka mwanzo wa Pleistocene)
-
Southern boobook
-
Barking owls
-
Morepork
-
Ochre-bellied hawk owls
-
Rufous owl
-
Brown hawk owl
-
Powerful owl
-
Laughing owl