Orso wa Loches (kwa Kilatini: Ursus; aliishi katika Ufaransa wa leo karne ya 6 hivi) alikuwa mmonaki aliyeanzisha monasteri mbalimbali, na hatimaye ile ya Loches aliyoiongoza kama abati hadi alipofariki [1].
Maarufu zaidi kati ya wafuasi wake alikuwa Leobasi.
Habari zake ziliandikwa na Gregori wa Tours.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |