Sinodi ya Whitby (664 BK) ilikuwa sinodi ya ufalme wa Northumbria ambapo Oswiu wa Northumbria aliamua kufuata desturi za Kanisa la Roma badala ya zile za Ukristo wa Kiselti zilizosambazwa awali kutoka Iona[1][2][3][4].
Sinodi hiyo ilifanyika kwenye monasteri pacha za Hilda wa Whitby huko Streonshalh (Streanæshalch), baadaye Whitby.