Monasteri ya Fontevraud yenye sehemu nne tofauti. Picha inaonyesha mbili tu.

Monasteri dabo ni makao ya wamonaki ambayo yana sehemu kwa wanaume na nyingine kwa wanawake, lakini kanisa ni la pamoja[1].

Mtindo huo ulianzia karne ya 4 katika Ukristo wa Mashariki [2] ukaenea Magharibi baada ya Kolumbani, lakini ulikatazwa na Mtaguso wa pili wa Nisea (787) [3]. Uamuzi huo ulichukua muda kutekelezwa, lakini mtindo huo ulijitokeza tena baada ya karne ya 12 hasa Uingereza chini ya Gilberti wa Sempringham.

Tanbihi

[hariri | hariri chanzo]
  1. Jankowski, Theodora A. (2000). Pure Resistance: Queer Virginity in Early Modern English Drama. University of Pennsylvania Press. uk. 65. ISBN 978-0-8122-3552-4.
  2. Lawrence 46.
  3. Hefele 385.

Marejeo

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Monasteri dabo kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.