Maelezo binafsi | |||
---|---|---|---|
Jina kamili | Mbwana Aly Samatta | ||
tarehe ya kuzaliwa | 23 Desemba 1992 | ||
mahali pa kuzaliwa | Dar es Salaam, Tanzania | ||
Maelezo ya klabu | |||
Klabu ya sasa | Fenerbahce | ||
Youth career | |||
2008–2010 | African Lyon | ||
Senior career* | |||
Miaka | Timu | Apps† | (Gls)† |
2010–2011 | Simba | ||
2011–2016 | TP Mazembe | ||
2016–2020 | K.R.C Genk | ||
2020– 2020 | Aston Villa | ||
Timu ya Taifa ya Kandanda‡ | |||
– | Tanzania | 17 | (6) |
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only. † Appearances (Goals). |
Mbwana Ally Samatta (alizaliwa 23 Disemba 1992), ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Tanzania katika klabu ya Feberbahce ya nchini Uturuki [1]. Mbwana ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na kabla ya kuhamia klabu ya Feberbahce (Uturuki) alikuwa akichezea timu ya Aston Villa ya nchini Uingereza[2].
Samatta alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya African Lyon mwaka 2008 ya nchini Tanzania. Alisajiliwa na klabu ya Simba S.C. mwaka 2010, ambapo alicheza katika nusu msimu tu kabla ya kujiunga na klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Alicheza kwa miaka mitano ndani ya TP Mazembe na kujijengea nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.
Mwaka 2015, alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka wa Afrika, na kumaliza msimu akiwa mfungaji bora wa mashindano ya klabu bingwa Afrika (Ligi ya Mabingwa Afrika) na kuisaidia klabu yake kushinda taji hilo.
Samatta alijiunga na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji mnamo januari 2016, aliisaidia kufuzu michuano ya Ulaya maarufu kama Europa Ligi na kushinda taji la ligi ya Ubelgiji (Belgian Jupiler Ligi mwaka 2019. Alimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo akashinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe award)[3].
Samatta alikua mchezaji muhimu wa TP Mazembe waliposhinda taji la klabu bingwa Afrika mwaka 2015 (2015 CAF Champions Ligi), akifunga jumla ya magoli saba na kumaliza akiwa mfungaji bora.[4]
Mnamo Januari 2016, aliposhinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutokea Afrika ya Mashariki kutwaa tuzo hiyo. Katika ugawaji wa tuzo hizo uliofanyika jijini Abuja, Nigeria, tarehe 7 Januari 2016, Samatta alikusanya jumla ya alama 127, akimzidi mchezaji mwenzake Robert Kidiaba mlinda lango wa TP Mazembe na timu ya taifa ya DR Congo aliyepata alama 88. Baghdad Bounedjah raia wa Algeria alishika nafasi ya tatu akiwa na alama 63.[5] Katika mchezo dhidi ya Moghreb Tétouan ya Moroko, Samatta alifunga magoli matatu kwa mpigo (hat-trick) yaliyowafanya wasonge hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika. Magoli hayo yanakumbukwa sana katika historia ya klabu ya TP Mazembe.[6]
Muda mfupi baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, alijiunga na klabu ya K.R.C. Genk kwa mkataba wa miaka minne na nusu.[7] Tarehe 23 Agosti 2018 Samatta alifunga goli tatu kwa mpigo(hat-trick) dhidi ya Brøndby IFkwenye mashindano ya Ulaya maarufu kwa jina la Europa Ligi walfanikiwa kupata ushindi wa goli 5–2.[8]
Mei 2019 aliishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe).
Mbwana Samatta ni Mndengereko kutoka Kibiti kwa kabila. Katika maisha ya imani ni Muislamu.[9]
Klabu | Msimu | Ligi | Cup | Kombe la ligi | Ya Bara | Mengineyo | Jumla | Ref. | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Ushindani | Michezo | Magoli | Michezo | Magoli | Michezo | Magoli | Michezo | Magoli | Michezo | Magoli | Michezo | Magoli | |||
Simba S.C. | 2010–11 | Ligi Kuu Tanzania Bara | 25 | 13 | — | Kigezo:Efn | 2 | — | 25 | 15 | [10][11] | ||||
TP Mazembe | 2011 | Linafoot | 8 | 2 | — | — | 8 | 2 | [10][11] | ||||||
2012 | 29 | 23 | — | 9 | 6 | — | 37 | 29 | [10][11] | ||||||
2013 | 37 | 20 | — | 5Kigezo:Efn | 5 | — | 42 | 25 | [10][11] | ||||||
2013–14 | 29 | 15 | — | 8 | 4 | — | 37 | 19 | [10][11] | ||||||
2014–15 | — | 6 | 4 | — | 6 | 4 | [11] | ||||||||
2015–16 | — | 6 | 4 | — | 6 | 4 | [11] | ||||||||
Jumla | 103 | 60 | 0 | 0 | 33 | 23 | 0 | 0 | 136 | 83 | – | ||||
K.R.C. Genk | Ligi kuu ya Ubelgiji | 6 | 2 | 0 | 0 | — | — | 12Kigezo:Efn | 3 | 18 | 5 | [12] | |||
2016–17 | 27 | 10 | 4 | 2 | — | 18 | 5 | 10Kigezo:Efn | 3 | 59 | 20 | [12] | |||
2017–18 | 20 | 4 | 4 | 0 | — | — | 11Kigezo:Efn | 4 | 35 | 8 | [12] | ||||
2018–19 | 28 | 20 | 1 | 0 | — | 12 | 9 | 10Kigezo:Efn | 3 | 51 | 32 | [12] | |||
Jumla | 81 | 36 | 9 | 2 | 0 | 0 | 30 | 14 | 43 | 13 | 163 | 65 | – | ||
Jumla maisha ya soka | 209 | 109 | 9 | 2 | 0 | 0 | 63 | 39 | 43 | 13 | 324 | 163 | – |
Taifa Stars | ||
Mwaka | Michezo | Magoli |
---|---|---|
2011 | 9 | 2 |
2012 | 4 | 0 |
2013 | 10 | 6 |
2014 | 3 | 1 |
2015 | 7 | 2 |
2016 | 4 | 1 |
2017 | 3 | 3 |
2018 | 5 | 2 |
2019 | 6 | 1 |
Total | 51 | 18 |
Goli | Tarehe | Uwanja | Mpinzani | Alama | Matokeo | Mashindano |
---|---|---|---|---|---|---|
1. | 26 Machi 2011 | Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Tanzania | Jamhuri ya Afrika ya Kati | 2–1 | 2–1 | kufuzu AFCON 2012 |
2. | 3 Septemba 2011 | Algeria | 1–0 | 1–1 | ||
3. | 11 Januari 2013 | Uwanja wa Adis ababa, Addis Ababa, Ethiopia | Ethiopia | 1–1 | 1–2 | Mchezo wa Kirafiki |
4. | 6 Februari 2013 | Uwanja wa Taifa Dar es Salaam | Kamerun | 1–0 | 1–0 | |
5. | 24 Machi 2013 | Moroko | 2–0 | 3–1 | kufuzu fainali za kombe la dunia 2014 | |
6. | 3–0 | |||||
7. | 4 Disemba 2013 | Uwanja wa Afraha, Nakuru, Kenya | Burundi | 1–0 | 1–0 | hatua ya makundi mashindano ya CECAFA 2013 |
8. | 12 Disemba 2013 | uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya | Zambia | 1–1 | 1–1 | mashindano ya CECAFA hatua ya mtoano 2013 |
9. | 3 Agosti 2014 | uwanja wa Estádio do Zimpeto, Maputo, Msumbiji | Msumbiji | 1–1 | 1–2 | Kufuzu AFCON 2015 |
10. | 7 Oktoba 2015 | Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania | Malawi | 1–0 | 2–0 | kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 hatua ya kwanza |
11. | 14 Novemba 2015 | Algeria | 2–0 | 2–2 | kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 – hatua ya pili | |
12. | 23 Machi 2016 | uwanja wa Stade Omnisports Idriss Mahamat Ouya, N'Djamena, Chad | Chad | 1–0 | 1–0 | kufuzu AFCON 2017 hatua ya makundi |
13. | 25 Machi 2017 | Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania | Botswana | 1–0 | 2–0 | Mchezo wa kirafiki |
14. | 2–0 | |||||
15. | 10 Juni 2017 | Lesotho | 1–0 | 1–1 | kufuzu AFCON 2019 Kundi L | |
16. | 27 Machi 2018 | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | 1–0 | 2–0 | Mchezo wa kirafiki | |
17. | 16 Oktoba 2018 | Cabo Verde | 2–0 | 2–0 | kufuzu AFCON 2019 | |
18. | 27 Juni 2019 | uwanja wa 30 June Stadium, Cairo, Misri | Kenya | 2–1 | 2–3 | AFCON 2019 Kundi C |
19. | 8 Septemba 2019 | Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania | Burundi | 1–0 | 1–1 (3–0 mikwaju ya penalti) | kufuzu michano ya kombe la dunia 2022 hatua ya kwanza |
TP Mazembe[13]
Genk
Binafsi
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mbwana Samatta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |