Kasuku | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Kasuku Mkia-mwekundu
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Familia 4; familia 2 na jenasi 8 katika Afrika:
|
Kasuku ni ndege wa oda Psittaciformes. Spishi za jenasi nyingine zinaitwa kwao au cherero. Kasuku wengine ni wakubwa, wengine wadogo. Wengi wana rangi kali. Wana mkia mrefu na miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Domo lao lina nguvu sana na mataya yamepindika kwa pande za kuelekea kama koleo. Kasuku wanatokea kanda zote za tropiki za dunia. Hula mbegu, kokwa, matunda na macho ya maua, pengine wadudu na wanyama wadogo pia. Spishi za “lories” na “lorikeets” hula mbochi na matunda mororo. Kasuku takriban wote hutaga mayai yao tunduni kwa mti.