Kanisa kuu la Kristo Mwokozi mjini Moscow
kwa Kirusi: Храм Христа Спасителя [Khram Khrista Spasitelya
Msalaba maalumu ya Kanisa hilo.
Patriarki Kirill I wa Moscow na Urusi wote.


Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi (kwa Kirusi: Ру́сская правосла́вная це́рковь|Rússkaya pravoslávnaya tsérkov) ndilo madhehebu kubwa zaidi ya Ukristo wa Mashariki, likiwa na waumini milioni 112, karibu nusu ya idadi ya Waorthodoksi wote duniani[1].

Pia ndilo Kanisa lililopatwa na dhuluma ya serikali iliyoua Wakristo wengi zaidi katika historia ya Kanisa.

Mkuu wake ndiye Patriarki wa Moscow na wa Urusi wote (kwa maana ya Russia, Ukraina[2] n.k.). Kwa sasa ni Kirill I.

Mwanzo na uenezi

[hariri | hariri chanzo]

Mwanzo rasmi wa Kanisa ni ubatizo wa Vladimir Mkuu, mtawala wa Kiev, uliotokea mwaka 988 kwa mikono ya mapadri kutoka Konstantinopoli walioleta mapokeo ya Ugiriki.

Warusi walipozidi kuenea katika Asia Kaskazini hadi Alaska, walieneza pia aina hii ya Ukristo iliyozaa matunda mengi, hasa kwa mchango wa umonaki, kiasi cha kufanya nchi iitwe Urusi Mtakatifu.

Dhuluma ndefu tena kali za Wakomunisti dhidi yake hazikuweza kufuta imani. Utawala wao uliposambaratika (1989), Kanisa lilistawi tena.

Takwimu zilizotolewa mwaka 2019 zinataja majimbo 314, maaskofu 382, parokia 38,649, mapadri 35,677, mashemasi 4,837, monasteri 972 na vyuo vya teolojia 30.[3]

Tanbihi

[hariri | hariri chanzo]
  1. Brien, Joanne O.; Palmer, Martin (2007). The Atlas of Religion. Univ of California Press. p. 22. ISBN 978-0-520-24917-2.
  2. "Religious tensions deepen Ukraine splits - Russian Orthodox official", Reuters, 16 May 2014. Retrieved on 5 March 2015. Archived from the original on 2015-09-24. 
  3. "Внутренняя жизнь и внешняя деятельность Русской Православной Церкви с 2009 года по 2019 год". Патриархия.ru.

Marejeo

[hariri | hariri chanzo]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.