Felisiani wa Foligno (San Giovanni Profiamma, karibu na Foligno, Umbria, Italia, 160 hivi - Foligno, 24 Januari 250 hivi) anayehesabika kuwa askofu wa kwanza wa eneo hilo lote kuanzia mwaka 204 hadi kifo chake [1].
Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 24 Januari[2].
Aliinjilisha mapema sehemu kubwa ya mkoa wa Umbria wa leo[3]-
Akiwa na umri wa miaka 90 hivi aliteswa kwa kukataa ibada kwa miungu ya Dola la Roma, akafa wakati wa kuburutwa kuelekea Roma kuuawa[4].
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |