Buruji za falaki (pia: alama za nyota; kwa Kiingereza: zodiac constellations) ni jina la makundinyota yanayoonekana kwenye ekliptiki zaani njia ya Jua angani (ing. ecliptic) na kuunda Zodiaki.
Katika maarifa ya unajimu (au: falaki, tofauti na fani ya sayansi inayoitwa astronomia) Waswahili wa kale, pamoja na tamaduni nyingi za zamani, waliamini ya kwamba nyota hizi zina tabia fulani na kuwa na athari juu ya maisha ya binadamu wanaozaliwa chini ya nyota fulani.
Hali halisi Jua linapita katika maeneo ya makundinyota 13 lakini tangu zamani za Babeli idadi ilifupishwa kuwa 12 kwa kusudi la kulingana na kalenda ya miezi 12. Kwa kufikia idadi hii kundinyota la Hawaa (Ophiuchus) liliondolewa katika idadi ya Zodiaki.
Kwa jumla majina mengi ya nyota yametokana na urithi wa falaki ya Waarabu. Hao walirithi habari hizi pamoja na mpangilio wa nyota kwenye mzingo wa njia ya jua angani kutoka Ugiriki ya Kale. Asili yake iko katika falaki ya Babeli.
"Buruji" yatokana na Kiarabu "برج", burj, tafsiri ya neno la Kigiriki πυργοι pirgoi, yaani mnara au boma[1].
Buruji za falaki katika utamaduni wa Waswahili ni kama zifuatazo:[2]
Katika unajimu wa siku hizi majina mengi ya kimapokeo katika unajimu wa Afrika ya Mashariki yamesahauliwa na badala yake wapiga falaki wanatumia orodha ya majina ambayo mara nyingi ni tafsiri ya majina ya Kiingereza tu, au pia namna ya kutaja alama ya makundinyota kwa neno la Kiswahili. Isipokuwa Mizani na Mashuke bado ni majina asilia. Majina katika unajimu wa kisasa jinsi yalivyo kawaida ni yafuatayo: