Mt. Batista.

Batista Varano, O.S.C. (9 Aprili 1458 - 31 Mei 1524) alikuwa binti wa mtawala wa Camerino. Baada ya kujitunza bikira na kuwa mfuasi wa Fransisko wa Asizi katika Utawa wa Mtakatifu Klara, akawa abesi wa monasteri iliyoanzishwa na baba yake.

Ni maarufu hasa kwa vipaji vyake katika sala, alipozama kwa uchungu katika mateso ya kiroho ya Yesu, pamoja na kupata faraja za kimbingu.

Alitangazwa na Papa Gregori XVI kuwa mwenye heri tarehe 7 Aprili 1843, akatangazwa na Papa Benedikto XVI kuwa mtakatifu tarehe 17 Oktoba 2010.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyoiaga dunia[1].

Ikulu ya baba wa Camilla huko Camerino, Marche, Italia.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Maandishi

[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri | hariri chanzo]
  1. Martyrologium Romanum

Marejeo

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.