Mt. Yohane Eudes alivyochorwa mwaka 1673.

Yohane Eudes (Ri, 14 Novemba 1601Caen, 19 Agosti 1680) alikuwa padri nchini Ufaransa.

Kwa miaka mingi alifanya kazi ya uinjilishaji katika parokia mbalimbali halafu akaanzisha shirika la Yesu na Maria kwa ajili ya malezi ya kipadri pamoja na lile la wamonaki wanawake wa Bibi Yetu wa Upendo kwa ajili ya kudumisha katika maisha ya Kikristo wale waliotubu[1].

Ndiye aliyetunga matini ya liturujia kwa sikukuu ya Moyo mtakatifu wa Yesu na ya Moyo safi wa Maria, ibada alizozihamasisha sana[2].

Alitangazwa na Papa Pius X kuwa mwenye heri tarehe 25 Aprili 1909, akatangazwa na Papa Pius XI kuwa mtakatifu tarehe 31 Mei 1925.

Sikukuu yake huadimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Maandishi yake muhimu zaidi

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/28900
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/28900
  3. Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.