Soko la Hisa la Dar es Salaam ni liko Dar es Salaam, mji mkubwa zaidi nchini Tanzania. Liliunganishwa mnamo Septemba 1996 na ununzi ulianza Aprili mwaka wa 1998; soko hili ni mwanachama wa Shirika la Masoko ya Hisa ya Afrika. Kwa sasa lina makampuni 11 yaliyoorodheshwa.
Ununuzi hufanyika kwa muda wa chini ya saa moja kwa kila juma[0].
Kifupisho | Kampuni | Maelezo |
1.DAHACO | Dar es Salaam Airports Handling Company | Shughuli za uchukuzi wa angani na majini |
2.EABL | East African Breweries | Bia, Gin, mvinyo |
3.KQ | Kenya Airways | Usafiri wa anga |
4.SIMBA | Tanga Cement | Saruji |
5.TBL | Tanzania Breweries | Inashirikiana na shirika la South African Breweries |
6.TCC | Tanzania Cigarette Company | Bidhaa za tumbaku, Sigara |
7.TOL | Tanzania Oxygen | Oksijeni, Nitrojeni, asetilini, gesi za dawa, vifaa vya kulehemu |
8.TATEPA | Tanzania Tea Packers | Chai na Kahawa |
9.TWIGA | Twiga Cement | Saruji |
10.NICOL | Taifa Investments Company Limited | Uwekezaji |
11.KCB | Kampuni ya Kenya Commercial Bank | Benki |
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Soko la Hisa la Dar-es-Salaam kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |