Salamu Maria (kwa Kilatini Ave Maria) kwa asili ni sala ya Wakatoliki wa Kanisa la Kilatini ambayo inamsifu Bikira Maria na kumuomba sala zake hadi saa ya kufa.
Sala hiyo imeenea hata kwa Wakristo wengine, hasa Waanglikana, lakini kwa namna tofauti inatumiwa pia katika Ukristo wa Mashariki.
Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya sala hiyo inatokana na Injili (Lk 1:28,42) moja kwa moja:
Katikati ya karne ya 13 sala ilikuwa inaundwa na maneno hayo tu pamoja na kuingiza jina la Maria, inavyoonekana katika ufafanuzi wa Thoma wa Akwino.[1]
Mwishoni mwa karne ya 15 yaliongezwa maneno ya kumuomba Maria sala zake.[2]
Hatimaye sala kwa Kilatini imekuwa hivi:
Tafsiri ya Kiswahili ni:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Salamu Maria kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |