Roland Brown alikuwa Mwingereza wa kwanza kuhudumu kama Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanganyika iliyokuja kuwa sehemu ya Tanzania baadaye.[1]
Brown alikuwa mkufunzi katika chuo cha Trinity College, Cambridge katika Chuo kikuu cha Cambridge, wakati wa harakati za uhuru wa Tanganyika; aliteuliwa kuwa mshauri mkuu wa Mwalimu Julius Nyerere.[2]
Mwaka 1961 aliteuliwa kuwa Mwanasheria mkuu wa kwanza baada ya uhuru wa Tanganyika.[3] Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyoangusha utawala wa kisultani, Brown aliteuliwa na Mwalimu Nyerere kuandaa hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.[4]
Mwaka 1965 alimaliza muda wake na nafasi yake ikachukuliwa na Mark Bomani.
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite book))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Roland Brown kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |