Richard Mganga Ndassa (21 Machi 1959 — Dodoma, 29 Aprili 2020) alikuwa mbunge wa jimbo la Sumve katika bunge la kitaifa nchini Tanzania.[1] Alitokea katika chama cha CCM.
Kabla ya kuingia bungeni Ndassa, aliyekuwa na cheti cha Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam, alikuwa meneja mauzo kwenye gazeti la Mfanyakazi kuanzia 1981 hadi 1996[2].