Raymond-Claude-Ferdinand Aron (14 Machi 190517 Oktoba 1983) alikuwa mwanafalsafa, mwanasosholojia, mwandishi wa habari na mtaalamu wa masuala ya siasa kutoka nchini Ufaransa.

Anafahamika pia kutokana na uhusiano wake wa muda mrefu wa kirafiki na wakati mwingine wa kiuhasama na Jean-Paul Sartre.[1]. Pia anafahamika zaidi kutokana na kitabu chake kilichotoka mwaka 1995, kilichofahamika kwa jina la The Opium of the Intellectuals.

Aron pia aliandika kwa undani kuhusu mada nyingine nyingi katika sosholojia, habari na filosofia. Akizungumzia kuhusu undani na ubora wa kazi za Aron, mwandishi na mwanahistoria James R. Garlan [2] ameandika kuwa, ijapokuwa anaweza kufahamika zaidi nchini Marekani, lakini Raymond Aron, anatajwa kuwa ni mtu maarufu sana miongoni wa wasomi wa nchini Ufaransa wa karne ya ishirini.

Maisha na kazi

Aron alizaliwa katika jiji la Paris, mzazi wake mmoja akiwa ni Mwanasheria, alisoma katika shule ya École Normale Supérieure, ambapo hapo alikutana na Jean-Paul Sartre, ambaye alikuja kuwa rafiki yake wa maisha na mpinzani wake mkubwa katika maswala ya elimu .[2]. Aron alishika nafasi ya kwanza katika mtihani wa Filosofia mnamo mwaka 1928, mtihani ambao rafiki yake wa karibu Sartre alishindwa kufaulu. na hatimaye mwaka 1930, alifanikiwa kutunukiwa shahada ya udaktari katika Historia ya Filosofia kutoka katika chuo cha École Normale Supérieure. Amekuwa akifundisha katika shule ya Social philosophy katika chuo kikuu cha Touloese, majuma machache kabla ya Vita vya Pili ya Dunia kuanza, halafu akaamia Armée de l'Air. Wakati nchi ya Ufaransa iliposhindwa katika vita hivyo, aliamua kuondoka nchini humo na kwenda London na kujiunga na vikosi vya Free French na baadae kuwa mhariri katika gazeti la France Libre (Free France). Baada ya vita kumalizika, Aron alirejea Paris kwa ajili ya kufundisha Sosholojia katika chuo cha École Nationale d'Administration na baadae Paris Institute of Political Studies. Hii ikiwa ni kati ya mwaka 1955 hadi 1968. Baadaye alienda kufundisha katika chuo kilichofahamika kama Sorbonne, na ilipofikia mwaka 1970, alihamia katika Collège de France. Alichaguliwa kuwa mwanachama mwenye hadhi ya juu katika taasisi ya American Academy of Arts and Sciences hii ikiwa ni mwaka 1960.[3] . Aron alifariki dunia katika jiji la Paris tarehe 17 Oktoba 1983 kwa shinikizo la moyo.

Kazi

Kazi nyingine

Bibliografia

Marejeo

  1. Memoirs: fifty years of political reflection, By Raymond Aron (1990)
  2. 2.0 2.1 Garland, James R. "Raymond Aron and the Intellectuals: Arguments supportive of Libertarianism." Journal of Libertarian Studies, Vol. 21, No. 3 (Fall 2007).
  3. Book of Members, 1780-2010: Chapter A. American Academy of Arts and Sciences. Iliwekwa mnamo 25 Aprili 2011.

Viungo vya nje