Papa Simako (kwa Kilatini: Symmachus) alikuwa Papa kuanzia tarehe 22 Novemba 498 hadi kifo chake tarehe 19 Julai 514[1]. Alitokea Sardinia, Italia[2] akaja kubatizwa Roma.
Alimfuata Papa Anastasio II akafuatwa na Papa Hormisdas.
Kwa muda mrefu alipaswa kukabili upinzani mkali wa antipapa Laurentius[3][4][5] na wafuasi wake wengi[6].
Alikomboa Wakristo waliofanywa watumwa na Wavandali na kusaidia waliokimbia dhuluma yao.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
|accessdate=
(help)
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Simako kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |