Papa Felix III alikuwa Papa kuanzia tarehe 13 Machi 483 hadi kifo chake tarehe 25 Februari/1 Machi 492[1]. Alitokea Roma, Italia, katika ukoo maarufu.
Alimfuata Papa Simplicio akafuatwa na Papa Gelasio I.
Uamuzi wake wa kwanza ulikuwa kukataa hati maarufu kama Henotikon kwa sababu haikusema wazi kwamba Yesu Kristo ana hali mbili, Umungu na utu [2]. Uamuzi huo ulisababisha farakano la Acacius wa Konstantinopoli.
Upande wa Afrika Kaskazini aliamua suala la Wakatoliki waliokubali kubatizwa tena na Waario ili kukwepa dhuluma ya watawala Wavandali[3]. Kufuatana na sinodi maalumu ya mwaka 487 aliwaandika maaskofu wa huko masharti ya kuwapokea upya kundini[4][5].
Kutokana na watoto aliowazaa katika ndoa yake kabla hajachaguliwa, walipatikana baadaye Papa Agapeto I (mjukuu) na Papa Gregori I (kitukuu)[6][7].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 1 Machi[8][9].
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Felix III kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |