Nyota na hilali ni ishara yenye historia ndefu inayochukuliwa leo mara nyingi kama ishara ya Uislamu [1]. Hii inatokana na matumizi yake katika bendera za Milki ya Osmani tangu karne ya 19[2]. Lakini historia yake ni ndefu na Waosmani waliipokea tayari kutoka milki ya Kikristo ya Bizanti.
Ishara hiyo ilianzishwa katika koloni la Kigiriki la Byzanti mnamo mwaka 300 KK. Ilitumika sana kama nembo ya kifalme ya mfalme wa Ponto Mithridate VI Eupator baada ya kuingiza Byzanti katika ufalme wake. [3]
Wakati wa karne ya 5, ilionyeshwa kwenye sarafu zilizotengenezwa na Milki ya Kiajemi ya Wasasani kwa zaidi ya miaka 400 kutoka karne ya 3 BK hadi kuanguka kwa Wasasani wakati wa uvamizi wa Waarabu Waislamu katika Uajemi (Iran).[4] Watawala Waislamu waliendelea kuonyesha alama hiyo kwenye sarafu zao wakati wa miaka ya mwanzo ya ukhalifa, maana sarafu hizo zilikuwa ni nakala halisi ya sarafu za Wasasani.
Ishara hiyo inaunganisha picha za mwezi hilali pamoja na nyota. Vipengele vyote viwili vina historia ndefu katika sanaa ya Mashariki ya Kati kama kuwakilisha ama Jua na Mwezi au Mwezi na Zuhura (nyota ya asubuhi) au sifa zao za kimungu.[5] [6][7]
Nyota mara nyingi huonyeshwa ndani ya upinde wa hilali. <ref>
((cite journal))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite journal))
: CS1 maint: date auto-translated (link)