Nikwata | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nikwata madoadoa (Hemidactylus brookii)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 12 za nikwata:
|
Nikwata ni spishi za mijusi-kafiri katika jenasi Hemidactylus ya familia Gekkonidae. Wamepewa jina hili kwa sababu huishi katika nyumba za watu mara nyingi. Spishi nyingine za Hemidactylus huitwa mijusi-kafiri vidole-majani na hawa wanatokea porini au msituni.
Kama mijusi-kafiri takriban wote nikwata hawana kope na hulamba macho mara kwa mara kuzuia yasikauke. Hukiakia usiku wakikamata wadudu.
Nikwata, na spishi nyingine zote za Hemidactylus, wana vidole vyenye ncha zilizopanuka (vidole-majani). Ncha hizi za vidole zinashika uso wowote, hata nyuso laini. Kwa hivyo wanaweza kutembea bila shida kwa ukuta na dari na hata kioo.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nikwata kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |