Lil Wayne.

Muziki wa hip hop ni aina ya muziki ulioanza kunako miaka ya 1970, ukiwa umeanzishwa na Wamarekani weusi katika miji mikubwa ya Marekani.

Hip hop mara nyingi inatumia staili moja ya kuimba iitwayo kurap au kufokafoka na ambayo mwimbaji anatoa au anaimba maneno-mashairi yaambatanayo na vina. Mashairi mengi yaliyoimbwa katika muziki wa hip hop yalikuwa yakizungumzia maisha halisi ya Watu weusi wa nchini Marekani, sanasana katika miji mikubwa.

Kuna baadhi ya mashairi ya muziki wa hip hop yanayozungumzia wahuni, uhalifu, na utumiaji haramu wa madawa ya kulevya.

Muziki wa hip hop pia huchukua tabia (mwenendo) wa staili za muziki wa pop, yaani kama disko na reggae.

Soma zaidi

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muziki wa hip hop kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.