Mlima Karelachgelat, ukiwa na kimo cha mita 3,350 juu ya usawa wa bahari, ni kilele cha sita[1] katika safu ya milima ya Cherang'any, iliyopo katika nyanda za juu magharibi mwa Kenya.
Vilima vya Cherangany huvuka kaunti tatu: kaunti ya Trans-Nzoia, kaunti ya Elgeyo-Marakwet na kaunti ya West Pokot na ni makazi ya jamii ya wawindaji-wakusanyaji iitwayo Wasengwer.
Vilima hivyo vina mmojawapo kati ya misitu mikubwa mitano ya Kenya na ni chanzo muhimu cha maji.
Tambarare yake kubwa ya kati imetenganishwa na mwambao wa Mau unaoinuka kuanzia kwenye mpaka na Tanzania mpaka Vilima vya Cherang'any. Mwambao huo unaonesha mwisho wa tambarare inayoinuka kwenye mteremko wa Mlima Elgon. [2]
Vilima vya Cherang'any viliundwa kutokana na mpasuko. Safu hizi huunda ubavu wa magharibi wa bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki lianzialo Jibuti kwa upande wa kaskazini hadi Msumbiji kwa upande wa kusini. Vilima vya Cherang'any vinapatikana kwenye mwambao wenye misitu na vimezingirwa na kuta za majabali kwenye pande tatu. Vilima hivyo vimeundwa kwa miamba na madini mbalimbali yakiwemo Chromite yaliyopatikana hapo na wanajiolojia kipindi cha ukoloni.[3][4]
Vilima vya Cherang'any vinasimamiwa na programu ya mazingira ya Umoja wa Mataifa kama mojawapo ya vyanzo muhimu vitano va maji nchini Kenya.[5] Kwa mujibu wa ripoti ya mwisho, iliyoonesha mabadiliko ya misitu katika vilima hivyo kati ya mwaka 2002 na 2003, ilionesha kuwa eneo hilo ni la mwisho kwa kuathirika kwa ukataji miti kati ya maeneo yote yaliyokuwa chini usimamizi. Huku ekari 174.3 zikiwa zimeharibiwa na ukataji miti, hasa katika kaunti za Elgeyo-Marakwet na Pokot Magharibi. Kwa sababu misitu hii ni ya uoto wa asili, ripoti hiyo inapendekeza paangaliwe kwa ukaribu ili kuepusha uharibifu zaidi.[6] Hifadhi hizo kumi na tatu za misitu huitwa Misitu ya vilima vya Cherang'any.
|url-status=
ignored (help)
|url-status=
ignored (help); Check date values in: |archivedate=
(help)
|url-status=
ignored (help); Check date values in: |archivedate=
(help)
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mlima Karelachgelat kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |