Mgunga (Vachellia spp.) | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mgunga mwavuli (Vachellia tortilis)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Migunga ni miti ya jenasi Vachellia katika familia Fabaceae yenye miiba mirefu kiasi na majani yenye sehemu nyingi. Zamani spishi hizi ziliainishwa katika jenasi Acacia lakini wanasayansi wamegawanya jenasi hii kwenye jenasi tano: Acacia, Vachellia, Senegalia, Acaciella na Mariosousa[1]. Spishi za Vachellia zina miiba miwili mirefu na nyofu kwenye kila kifundo. Miti hii inatokea maeneo kavu ya Afrika, Amerika, Asia, Australia na Ulaya (imewasilishwa).