Mfalme Henry I na Matilda, kutoka Chronica sancti Pantaleonis, karne ya 12.

Matilda wa Ringelheim (kwa Kijerumani Mathilde von Ringelheim; 894/89714 Machi 968) alikuwa malkia mdogo wa Saxony kuanzia mwaka 912 na malkia wa Ujerumani mzima kuanzia mwaka 919 kutokana na ndoa yake na Henry I, mfalme wa kwanza wa nasaba ya Otto.

Mke mwaminifu kabisa, alikuwa na unyenyekevu na subira sana; pia alijitahidi kusaidia watu fukara na kujenga hospitali na monasteri.

Baada ya kufiwa mumewe mwaka 936, alianzisha abasia ya Quedlinburg kwa heshima yake. Matilda aliishi hadi kuona Dola la Roma la Magharibi kuanzishwa tena na mwanae wa kwanza, Otto I aliyetiwa taji mwaka 962.

Baada ya hapo alikwenda kutawa katika abasia hiyo ambapo ndipo alipofariki.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake, 14 Machi[1].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri | hariri chanzo]
  1. Martyrologium Romanum

Vyanzo

[hariri | hariri chanzo]

Marejeo

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Matilda wa Ringelheim
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.