Mantiki (kutoka Kiarabu منطق mantiq; kwa Kiingereza logic kutoka Kigiriki logos, yaani neno, wazo) ni elimu jinsi ya kutoa hoja sahihi.

Mantiki inasaidia kufikia uamuzi kama hoja fulani ni ya kweli au la. Mantiki ni tawi la falsafa, pia hisabati.

Mfano wa hitimisho (syllogism) kutoka Wagiriki wa Kale na siku za mwanzo wa mantiki iliyotolewa na Aristoteli:

  1. Kila mtu atakufa
  2. Sokrates ni mtu
  3. Kwa hiyo Sokrates atakufa

Mantiki kwa fomula

Hitimisho hiyo inaweza kuandikwa pia kwa fomula:

Kwa hiyo hitimisho ya Aristoteli kwa fomula:

Hiyohiyo kama fomula kwa mifano yote: