Kipindi cha njiamzingo ni muda ambao kiolwa cha angani kinachukua ili kumaliza njiamzingo moja kuzunguka kiolwa chengine. Katika elimuanga, huhusika na sayari au visayari vizungukavyo Jua, miezi izungukayo sayari, sayari-nje zizungukazo nyota nyingine, au nyota maradufu. Pia huhusika na muda ambapo satelaiti au vipimaanga vinamaliza njiamzingo moja kuzunguka kiolwa cha angani.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kipindi cha njiamzingo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.