Kata ya Kiborloni | |
Mahali pa Kiborloni katika Tanzania |
|
Majiranukta: 3°20′24″S 37°20′24″E / 3.34000°S 37.34000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Kilimanjaro |
Wilaya | Moshi Mjini |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 9,202 |
Kiborloni ni kata ya Moshi Mjini katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania, yenye postikodi namba 25113.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,202 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,206 [2] walioishi humo. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ina wakazi wapatao 7,028 waishio humo. [3]
Wananchi wa kata hii wanajishughulisha na biashara ndogondogo kama uuzaji wa mbogamboga na matunda na pia wanajishughulisha na zao la ndizi. Makabila yafuatayo yanapatikana katika kata hiyo: Wachagga, Wapare, na mengineo mengi.
Ndani ya kata hii ya Kiborloni kuna ikulu ndogo ambayo Rais huwa anaitumia kwa ajili ya mapumziko akiwa na ziara katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Kata za Wilaya ya Moshi Mjini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania | ||
---|---|---|
Bomambuzi | Bondeni | Kaloleni | Karanga | Kiborloni | Kilimanjaro | Kiusa | Korongoni | Longuo B | Majengo | Mawenzi | Mfumuni | Miembeni | Mji Mpya | Msaranga | Ng'ambo | Njoro | Pasua | Rau | Shirimatunda | Soweto |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kiborloni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|