Khoikhoi (au Khoekhoe[1]; kwa lugha yao maana ni "watu watu", "watu halisi"[2] [3]) ni wakazi asili wa Kusini mwa Afrika pamoja na Wasan, ambao kwa jumla wanaitwa Khoisan.
Tofauti kati yao ni hasa utamaduni, kwa maana Wasan (kwa maana halisi "Wagunduzi").[4] wanaendelea kwa kiasi kikubwa kuishi kwa uwindaji, wakati Khoikhoi toka muda mrefu wanategemea ufugaji wa kuhamahama na kilimo[5].
Kadiri ya akiolojia walifikia eneo la Cape Town miaka 2,000 iliyopita wakitokea kaskazini (Botswana ya leo).
Kuanzia karne ya 3 BK walifikiwa na wavamizi wa Kibantu waliojitwalia maeneo mazuri zaidi.
Ingawa ni wazi kuwa uwepo wa Khoekhoen Kusini mwa Afrika unatangulia upanuzi wa Wabantu, kulingana na nadharia ya kisayansi inayotokana na ushahidi wa kilugha, haijulikani ni lini Wakhoekhoe walianza kukaa katika maeneo ambayo mawasiliano ya kwanza na Wazungu yalitokea (labda katika Umri wa Jiwe la kale).[4] Wakati huo, katika karne ya 17, Wakhoekhoe walitunza ng'ombe wengi wa aina ya Nguni katika mkoa wa Cape. Ufugaji wao wa kuhamahama uliachwa zaidi katika karne ya 19 hadi ya 20.[6]
The nomadic pastoral Khoikhoi kraals were dispersed and their organization and culture broken. However, their successors, the trekboers and their Khoikhoi servants, managed flocks and herds similar to those of the Khoikhois. The trekboers had adapted to African-style, extensive pastoralism in this region. In order to obtain optimal pasture for their animals, early settlers imitated the Khoikhoi seasonal transhumance movements and those observed in the larger wild herbivores.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Khoikhoi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |