Isotopi 3 za hidrojeni

Isotopi (pia: nyukilidi) ni aina tofauti za atomi za elementi za kikemia. Isotopi za elementi fulani zina nambari sawa ya protoni katika viini vyao lakini nambari tofauti za neutroni.

Atomi ya elementi ya kikemia inaweza kupatikana kwa hali tofauti. Hali hizi tofauti huitwa isotopi.

Isotopi, protoni, elektroni na nyutroni

Atomi zote za elementi moja ziko sawa katika

Isotopi za elementi moja zinatofautiana katika

Tabia za elementi kikemia na kifizikia

Hali ya isotopi haibadilishi tabia za elementi na hapo ni asili ya jina "iso-topi" kutoka Kigiriki isos (ἴσος "sawa") na topos (τόπος "mahali"). Maana yake hata kama atomi hizi zina tabia tofauti za ndani zinapangwa mahali palepale kwenye jedwali la elementi. Ilhali tabia za nje za atomi zinatawaliwa na idadi ya elektroni katika mizingo elektroni, isotopi hazionyeshi tofauti kikemia lakini kwa macho ya fizikia zinaweza kuwa tofauti. Kwa hiyo hata isotopi za elementi zinajenga molekuli sawa na atomi zote za elementi hii. Lakini michakato ya muungo atomia inaendelea polepole kiasi kama masi ya isotopi ni kubwa zaidi.

Aina za isotopi

Elementi zote zinajulikana kuwa na isotopi, kuanzia moja hadi nyingi. Isotopi zinaweza kutofautishwa kwa makundi mawili:

Katika viini atomia vya isotopi thabiti kuna uwiano kati ya nyutroni na protoni. Halafu hakuna nguvu inayosababisha badiliko la atomi ndani yake.

Mbunguo nyuklia wa isotopi nururifu

Katika kiini cha atomi za isotopi nururifu uwiano kati ya nyutroni na protoni si thabiti. Uwiano huu haupo. Atomi hizi zinaelekea kuingia katika hali ya uwiano kwa kupunguza chembe au nishati. Huu ni mnururisho na kuna hasa aina tatu za mnururisho zinazoitwa kwa herufi za Kigiriki alfa, beta na gamma. Mchakato huu unaitwa mbunguo nyuklia. Kwa njia ya mnururisho alfa na beta atomi inaachana na chembe kadhaa na kuwa elementi nyingine katika hali thabiti.

Kwa mfano Kaboni (C) inapatikana kiasili kwa umbo la isotopi tatu.