Godbless Jonathan Lema (amezaliwa 26 Oktoba 1976) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CHADEMA. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Arusha Mjini kwa miaka 2015-2020. [1][2]
Godbless Lema alianza siasa zake mwaka 2005, kipindi hicho akiwa mwanachama wa chama cha TLP.
Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 alipata hifadhi ya kisiasa kwanza nchini Kenya, halafu Kanada[3].