2°52′29″S 32°13′45″E / 2.874783°S 32.229218°E
Geita ni mji na makao makuu ya mkoa wa Geita iliyopata halmashauri yake ya pekee mnamo mwaka 2012[1].
Mji wote huwa na eneo la kilomita za mraba 1080 na maeneo yake yalitengwa na Wilaya ya Geita.
Msimbo wa posta ni 30101. [2]
Mnamo mwaka 2015 idadi ya wakazi wa Geita mjini ilikadiriwa kuwa na watu 192,541[3] Mwaka 2022 walihesabiwa 361,671 [4].
Uchumi wa Geita na kuukua kwa mji umetegemea upatikanaji wa dhahabu katika miamba ya mazingira. Uchimbaji unatekelezwa na wachimbaji wadogo na kampuni ya AngloGold Ashanti inayoajiri watu 5,000[5].
Kata za Mji wa Geita - Mkoa wa Geita - Tanzania | ||
---|---|---|
Bombambili | Buhalahala | Bulela | Bung'wangoko | Ihanamilo | Kalangalala | Kanyala | Kasamwa | Mgusu | Mtakuja | Nyanguku | Nyankumbu | Shiloleli |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Geita bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |