Fulgensyo wa Ruspe (Fabius Claudius Gordianus Fulgentius[1]; Thelepte, leo Medinet-el-Kedima, 462 au 467 – Ruspe, 1 Januari 527 au 533) alikuwa mmonaki, mwanateolojia na askofu wa Ruspe (leo nchini Tunisia)
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[2].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].
Mtoto wa familia tajiri[4], alijifunza vizuri kabisa Kigiriki na pia Kilatini[4].
Kwa jinsi alivyosimamia familia yake alipata sifa na kazi ya liwali huko Afrika Kaskazini. Hata hivyo aliacha mapema awe mmonaki[5].
Mwaka 499 hivi aliondoka ajiunge na wakaapweke wa Thebais huko Misri, lakini alikata tamaa aliposikia juu ya wamonaki wa huko kuathiriwa na mafundisho mapotofu ya Eulalius, askofu wa Siracusa.[6] Badala yake alianzisha monasteri huko Byzacena chini ya askofu Faustus, bila kujali udhaifu wa mwili wake wala upinzani wa mama yake.[7]
Waario walipozidi kushambulia eneo hilo, Fulgensyo alilazimika kuhamia monasteri ya jirani, halafu Sicca Veneria alipokamatwa na kuteswa kwa imani yake Katoliki.
Mwaka 500 alihiji Roma, kwenye makaburi ya Mitume Petro na Paulo, halafu arakudi Byzacena, alipojenga monasteri, akichagua kuishi peke yake chumbani.
Sifa yake ilienea akapewa mara kadhaa nafasi ya uaskofu katika majimbo yaliyopungukiwa kutokana na dhuluma ya mfalme Thrasamund wa Wavandali.[7] Hatimaye mwaka 502 Fulgensyo alikubali kuongoza Wakristo wa Ruspe.[6]
Maadili yake yaligusa sana waumini, lakini mfalme alimfukuza pamoja na maaskofu wengine sitini wasiokubali Uario wakaishi katika kisiwa cha Sardinia alipopewa kila mwaka msaada wa Papa Symmachus. Akiwa huko, aligeuza nyumba yake mjini Cagliari kuwa monasteri, akaanza kuandika vitabu kwa ajili ya Wakristo wa Afrika.
Kwa amri ya mfalme, mwaka 515 alirudi barani kwa ajili ya mhadhara na Mwario aliyeshika jimbo lake. Kitabu chake, Jibu la Hoja Kumi zilizotolewa dhidi ya Kanuni ya Imani ya Nisea kilimshtua Thrasamund hata akakatazwa kauli za Fulgensyo zisitolewe tena kwa maandishi. Lakini yeye aliongeza Vitabu Vitatu kwa Mfalme Thrasamund. Mfalme huyo alizidi kumheshimu Fulgensyo akamruhusu kuishi Karthago, lakini mwaka 520 akamrudisha Sardinia.
Fulgensyo alianzisha jumuia mbalimbali Afrika Kaskazini na Sardinia.[8]
Mwaka 523, baada ya kifo che Thrasamund, aliingia madarakani mwanae Hilderic, aliyekuwa Mkatoliki. Hivyo Fulgensyo aliruhusiwa kurudi Ruspe akajitahidi kuvuta wananchi wote katika Kanisa Katoliki na kurekebisha hali mbaya iliyoenea jimboni mwake alipokuwa mbali.[9]
Baadaye Fulgensyo alirudi kuishi monasterini katika kisiwa cha (Kerkenna), lakini akarudishwa tena Ruspe, alipohudumia hadi kifo chake tarehe 1 Januari 527[6] or 533.[4]
Kati ya maandishi yake zimetufikia barua kadhaa na hotuba nane.
((cite web))
: Unknown parameter |=
ignored (help); Unknown parameter |deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite web))
: Unknown parameter |=
ignored (help)
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |