Fatma Hassan Toufiq (amezaliwa 29 Februari 1960) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha [[Chama Cha Mapinduzi] (CCM). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti maalum vya wanawake kwa miaka 2015 – 2020. [1]
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Mtekelezo (1967-1973) na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Central (1974-1977). Alipata cheti cha ualimu katika Chuo cha ualimu Marangu (1979-1981) na (2009-2013) alisomea shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na shahada ya uzamili (2014-2016) katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. [2]