Fatma Abdulhabib Fereji (amezaliwa 26 Julai 1961) ni mbunge katika baraza la wawakilishi la Zanzibar, Tanzania.[1] kupitia chama cha Civic United Front (CUF).
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Darajani kuanzia mwaka 1967 hadi 1973 na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Hamamni (1974-1976) na kuhamia katika katika Chuo cha Lumumba kwa ajili ya masomo ya sekondari ngazi ya awali na mwisho kuanzia (1977-1980) na baadae alipata shahada ya kwanza ya Ualimu wa sanaa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1983-1986) na shahada ya uzamili ya ukutubi katika chuo kikuu cha Wales, Ufalme wa Muungano (1989-1991)[2]