Chura wa Kihansi | |
---|---|
Kihansi spray toad at the Toledo Zoo | |
Hali ya hifadhi
| |
CITES Appendix I (CITES)[2]
| |
Uainishaji wa Kisayansi | |
Himaya: | Animalia |
Faila: | Chordata |
Class: | Amphibia |
Oda: | Anura |
Familia: | Bufonidae |
Jenasi: | Nectophrynoides |
Spishi: | N. asperginis
|
Jina la kibiolojia | |
Nectophrynoides asperginis Poynton, Howell, Clarke & Lovett, 1999
|
Chura wa Kihansi (Nectophrynoides asperginis, Kihansi Spray Toad) ni chura mdogo aliye kienyeji katika eneo la Kihansi, Tanzania pekee.[3] [4] Spishi hiyo inazaa hai na inakula wadudu. [3] Mwaka 1999 mazingira asili yaliathiriwa na ujenzi wa Lambo la Kihansi. Chura wa Kihansi kwa sasa ameainishwa kama aliyetoweka porini lakini spishi hii inaendelea nje ya eneo lake la asili ikitunzwa katika hifadhi.
Kiasili chura huyu alipatikana pekee katika eneo dogo la hekta 2 (ekari 5) chini ya maporomoko ya maji ya Mto Kihansi katika mtelemko wa Udzungwa kwenye Mkoa wa Iringa nchini Tanzania. [5] Korongo la Kihansi lina urefu wa kilomita 4 likielekea kaskazini-kusini. [6]
Manyunyu ya maporomoko yaliunda mlia mwembamba mwenye mazingira ya pekee yaliyokuwa nyumbani wa chura huyu.[6] Ardhi nyevu hizi zilikuwa na uoto mnene wenye nyasi ikiwa ni pamoja na nyasi za Panicum, Selaginella kraussiana na kangaga (Tectaria gemmifera). [6] Maeneo ndani ya maeneo ya kunyunyizia maji ya maporomoko ya maji yalikuwa na halijoto isiyobadilika sana na unyevu wa 100%. [6]
Tangu kujengwa kwa lambo la Kihansi kwenye mwaka 1999 mfumo wa kunyunyizia uliwekwa kwa shabaha ya kutunza uhai wa chura unaolenga kuiga hali ya kiasili. Lakini mamlaka ulichelewa kuweka mfumo huu mapema[7] na chura zote za eneo hili walitoweka katika muda wa miaka michache.
Chura wengine wa spichi hiyo walitafutwa katika mazimgira ya maporomoko mengine ya maji kwenye miinuko ya Milima ya Udzungwa lakini hawakupatikana. [8]
Mpango wa ufugaji mbali na eneo la asili ulianzishwa mnamo mwaka 2001 kwa lengo la kuhifadhi spishi hiyo. Chura 500 walichukuliwa Kihansi na kupelekwa zoo sita.[9] [10] [11] Zoo mbili pekee za Bronx na Toledo ndizo zilizoweza kudumisha idadi ya chura. [10] Kwa sasa Toledo kuna vyura elfu kadhaa wa Kihansi, [9] [12] wengi wao wakiwa nje ya maonyesho. Zoo ya Bronx pia ina vyura elfu kadhaa wa Kihansi. [12]
Tangu Agosti 2010 vyura kadhaa walirudishwa katika mazingira asili huko Kihansi kutoka Marekani[9] kwa kutumia kituo cha uenezi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. [11] [13] Kuna hatari kutokana na fungus fulani (chytrid fungus) inayoua vyura wengi[14].
Watafiti wanaona kwamba kuletwa tena kwa spishi hiyo porini kunaweza kuchukua muda kwa sababu inahitaji kuzoea mazingira ya porini ambayo inahitaji kutafuta chakula, kukwepa wanyama wanaowinda wanyama wengine, na kushinda magonjwa, tofauti na mazingira yaliyodhibitiwa ambayo waliishi wakati wa kufugwa Marekani. [15]
Tangu mwaka 2020 Shirika la Umeme Tanesco lilishiriki katika gharama za utunzaji wa vyura hao na kuwarudisha tena Tanzania kwa jumla ya TSh milioni 611.92[16]
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite journal))
: |hdl-access=
requires |hdl=
(help)
<ref>
tag; no text was provided for refs named :0
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref>
tag; name "Toledo" defined multiple times with different content
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chura wa Kihansi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |