Catherine Valentine Magige (alizaliwa mkoani Arusha 8 Mei 1981) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CCM. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti maalum vya wanawake kwa miaka mitano (2015 – 2020 [1]). Amehitimu katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Kimandolu kuanzia 1989-1995 na elimu ya sekondari katika shule wa wasichana Ngarenaro kuanzia 1996-1999.[2].
Mwaka 2014 alikuwa mwakilishi katika bunge la Katiba [3]