Bukabwa ni kata ya Wilaya ya Butiama katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31205[1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,002 waishio humo.[2]

Kata ya Bukabwa inajumuisha vijiji vya Bukabwa yalipo makao makuu ya kata, Mmazami na kirumi, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kata ya Bukabwa ina wakazi wapatao 11,002 kwa mchanganuo ufuatao; kijiji cha Bukabwa kina wakazi wapatao 3,127, kijiji cha Kirumi wakazi 3,291 na kijiji cha Mmazami kina wakazi 4,584.

Idadi kubwa ya kata hii inakaliwa na jamii ya Wakabwa, na kiasi kidogo jamii ya Wazanaki, Wakiroba na Wasimbiti. Mwaka wa 2014 kijiji cha Bukabwa kilipata umeme kupitia mradi wa umeme vijijini unaodhaminia na serikali ya Tanzania kupitia wakala wa umeme vijijini (Rural energy Agent-REA).

Marejeo

  1. https://www.tcra.go.tz/images/documents/postcode/mara.pdf[dead link]
  2. Sensa ya 2012, Mara - Butiama-District-Council
Kata za Wilaya ya Butiama - Mkoa wa Mara - Tanzania

Bisumwa | Buhemba | Bukabwa | Buruma | Busegwe | Buswahili | Butiama | Butuguri | Bwiregi | Kamumegi | Kukirango | Kyanyari | Masaba | Mirwa | Muriaza | Nyamimange | Nyankanga | Sirorisimba


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bukabwa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.