Athi River Mining (kifupi ARM) ni kampuni ya kibiashara nchini Kenya inayochimba madini na kutengeneza bidhaa kama saruji, mbolea wa kilimo, aina kadhaa za chokaa na minerali mingine kwa matumizi ya viwandani na katika ujenzi.

Kampuni ilianzishwa na Bwana H.J. Paunrana mwaka 1975 mjini Athi River na makao makuu yake yapo Nairobi. Kiasili iliana kuchimba mawe ya chokaa katia eneo la Athi River na kuusafisha, kusaga na kuuza.

ARM ina migodi na viwanda katika Kenya, Tanzania na Afrika Kusini.

ARM inajenga kituo cha umeme cha makaa chenye nafasi ya megawati 29 huko Kaloleni/Mombasa kwa shabaha ya kupunguza gharama zake za nishati na kuuza umeme wa ziada kwenye soko la kitaifa.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]