2012 DA14 ni asteroidi lenye mzingo wa kukaribia dunia.
Imekadiriwa kuwa na kipenyo cha mita 50 na masi ilikadiriwa kuwa tani 190,000.
Astroidi hii ilitazamiwa mara ya kwanza mwaka 2012 na wanaastronomia kwenye paoneaanga pa La Sagra. Hapo mwanzoni kulikuwa na hofu ya kwamba asteroidi hii inaweza kuwa na hatari maana kama ingegongana na dunia ingesababisha hasara nyingi sawa na nguvu ya bomu ya kinyuklia jinsi ilivyotokea mwaka 1908 huko Tunguska. [1]
2012 DA14 ilipita karibu na dunia tarehe 15 Februari 2013 kwa umbali wa kilomita 27,700 yaani ndani ya obiti ya Mwezi na hata ndani ya obiti ya satelaiti za mawasiliano. [2]
Jinsi ilivyotabiriwa na wataalamu iilipita salama bila hatari ya muanguka chini na kugonga dunia. Hata hivyo mpito wake ulikuwa mpito wa karibu kabisa wa gimba lenye ukubwa wake ulioweza kupimwa..
Mpito ujao wa karibu utatokea mwaka 2046 lakini unatabiriwa kuwa na umbali zaidi kuliko mwaka 2013.